ISIS waweka mitego kulinda mji wa Mosul

Haki miliki ya picha AP
Image caption ISIS waweka mitego kulinda mji wa Mosul

Kundi la wanamgambo wa Islamic State limeunda mitego ardhini, mahandaki na vizuizi vya barabarani katika mji wa Mosul nchini Iraq ili kuulinda mji huo kutokana na mashambulio ya aina yoyote kutoka kwa majeshi ya serikali.

Uchunguzi wa BBC kuhusiana na maisha ya raia mjini Mosul mwaka mmoja baada ya kutekwa na Islamic State umebaini kuwa kundi hilo sasa linadhibiti kila kitu mjini humo, kuanzia sare za wanafunzi wa shule napia kuwapa wanafunzi mafunzo ya itikadi kali.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption ISIS waweka mitego kulinda mji wa Mosul

Matumizi ya simu za mkononi haikubaliwi huku habari zikidhibitiwa na kundi hilo linalojiita pia Dayesh.

Waislamu wa madhehebu ya Shia wameuawa,huku maeneo ya mji huo ambapo zamani kulijaa watu sasa yamesalia mahame.

Maeneo ya kitamaduni na ya kale Mjini Mosul yameharibiwa au kubadilishwa huku misikiti mikubwa maarufu ikibomolewa.