Watawa wakwama ndani ya lifti kwa siku 3

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watawa wakwama ndani ya lifti kwa siku 3

Watawa wawili wameokolewa kutoka kwa lifti mjini Rome baada ya kukwama kwa siku tatu bila chakula wala maji.

Wawili hao mmoja wa miaka 69 raia wa New Zealand na mwingine wa umri wa miaka 58 raia wa Ireland walikwama ndani ya lifti hiyo siku ya Ijumaa baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme.

Watawa hao waligunduliwa siku ya Jumatatu wakati mfanyikazi mmoja kuwaita polisi, alipokosa kujibiwa baada ya kufinya kengele ya mlango.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Watawa wakwama ndani ya lifti kwa siku 3

Wakati polisi walipoingia kwenye nyumba hiyo, waliita kutaka kujua ikiwa kulikuwa na mtu ndipo watawa hao wakaitika wakisema kuwa wako ndani ya lifti.

Walipotolewa walisema kuwa waliomba sana. Kisha walipekwa hospitali iliyo karibu ambapo walipata matibabu.