Al Shabaab ladai kuwaua askari wa Ethiopia

Image caption Al shabaab

Kumekua na mapigano makali katikati mwa Somalia baina ya wanajeshi wa taifa hilo ,wanamgambo wa kiislam wa Alshaabab na wanajeshi wa Ethiopia

Al Shabaab linasema limewauwa askari 30 wa Ethiopia ambao ni sehemu ya kikosi cha muungano wa Afrika na kuharibu magari saba ya kijeshi .

Watu katika kijiji cha Jame kilichopo karibu na mji wa Bur Hakaba wanasema kuwa walisikia milio ya risasi.

Hakuna ripoti yoyote kutoka kwa serikali ya Ethiopia kufikia sasa.

Kundi la alshabaab limefurushwa katika miji mingi ya Somalia lakini bado linadhibiti maeneo mengi ya mashambani.