Vyama 17 kususia uchaguzi Burundi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Burundi

Kundi moja la vyama 17 nchini Burundi limekubaliana kususia uchaguzi mkuu wa mwezi ujao likisema kuwa hautakuwa huru na haki.

Upinzani unasema kuwa rais Pierre Nkurunziza hafai kuwania muhula wa tatu.

Pia wanataka uchaguzi huo kuahirishwa ,msimamo unaoungwa mkono na viongozi wa eneo hili.

Taifa la Burundi limekumbwa na maandamano na majaribio ya mapinduzi yaliofeli tangu rais Pierre Nkurunziza kutangaza mwezi Aprili kwamba atawania muhula mwengine.