Afrika yatakiwa kutotegema misaada

Image caption Ujumbe wa Twitter wa rais Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema wakati umefika kwa mataifa ya Afrika kukoma kutegemea misaada kutoka mataifa ya nje.

Kwenye ujumbe alioutuma katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter, rais Kenyatta amesema misaada hiyo ya kigeni mara nyingi huwa na vikwazo na masharti ambayo yanakandamiza.

Ameongeza kusema kuwa hatma ya bara la afrika siku zijazo haipaswi kuwa mikononi mwa mataifa ya magharibi ambayo mara nyingi huweka maslahi yao kwanza.

Kenya hutegemea mabilioni ya dola kila mwaka yanayotolewa na mataifa ya kigeni na katika bajeti ya mwaka wa 2015-16 waziri wa fedha wa Kenya alijumuisha misaada kutoka nje katika makisio ya serikali ya mwaka huu.