Shirika la ndege taabani kwa kupakua mjusi

Image caption Mjusi apatikana ndani ya mlo wa abiria India

Magazeti nchini India yameripoti kisa cha kutamausha kilichotokea katika ndege ya shirika la Air India.

Abiria mmoja aliyekuwa safarini kuelekea mjini London Uingereza akitumia ndege ya shirika la ndege ya Air India alizua hofu miongoni mwa abiria wengine alipopiga kamsa kwa mshtuko baada ya kumpata mjusi kafiri ndani ya mlo wake.

Abiria wote walitamauka wasijue kilichompata mwenzao haswa wakati huu ambapo kunataharuki kubwa na tahadhari kuhusiana na maswala ya usalama kufuatia matukio ya ugaidi kote duniani.

Mjusi kwenye mkate

Bwana huyo ambaye awali alikuwa ameagiza chakula maalum kutoka kwa mhudumu wa ndege hakuamini macho yake alipokaribia kumla mjusi macho makavu !

Inasemekana kuwa alipofungua mkate wake akitaka kuunga'ta mara akaona ukitikisika .

Ghafla bin vu akaona mjusi akijifurukuta akitafuta njia ya kujinasua kutoka kwenye plastiki iliyokuwa imefunika chakula chake.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Alipiga mayowe kwa sauti ya juu usingeliamini kuwa ni mwanaume.

Alipiga mayowe kwa sauti ya juu usingeliamini kuwa ni mwanaume.

Shirika hilo limekanusha habari hiyo japo kuna picha inayoendelea kusambazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ikionesha mjusi mdogo kwenye mkate .

Waziri wa usafiri wa anga ametao onyo kwa shirika hilo akisema kuwa halifai kuwapakulia wateja wake mijusi !

Maoni yako

Ungefanyaje wewe ?

Tuachie maoni yako kwenye mtandao wetu wa Twitter na ule wa Facebook.

Tafuta BBCSwahili ugonge like kisha utuachie maoni yako!