Homa ya MERS yasambaa Korea Kusini

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Homa ya MERS yasambaa Korea Kusini

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa mlipuko wa homa ya Middle East Respiratory Syndrome au MERS nchini Korea Kusini na mkubwa na huenda kesi zaidi zikaripotiwa.

Baada ya uchunguzi wa wiki moja shirika la WHO linasema kuwa madaktari nchini korea kusini ambao hawakuhufahamu ugonjwa huo huenda walichangia ugonjwa usambae kwa haraka .

Utawala nchini korea kusini unasema kuwa watu 12 wameambukizwa ugonjwa wa MERS huku 14 wakijulikana kuaga dunia.