Mwanamfalme Philip amuoa muigizaji Sweden

Image caption Mwanamfalme Philip amuoa muigizaji Sweden

Mamia ya watu wamejitokeza mabarabarani mjini Stockholm Sweden kushuhudia harusi ya mwanamfalme Prince Carl Philip na muigizaji nyota na mwanamitindo wa zamani bi Sofia Hellqvist.

Harusi yao ilifanyika leo adhuhuri katika makao ya kifalme mjini Stockholm.

Image caption Walikutana 2010 katika mkahawa

Wawili hao walijitokeza mabarabarani katika mkokoteni unavutwa na farasi wakiwasalimia wafuasi wao.

Sofia Hellqvist, 30, alikuwa mkufunzi wa yoga na mwanamitindo kabla ya kuanzisha shirika lisilokuwa la kiserikali.

Image caption Bi harusi aliwahikuwa mwanamitindo wa majarida ya wanaume

Mumewe 36 Carl Philip, Mwanamfalme ni watatu katika orodha ya familia ya kifalme mwenye uwezo wa kutawala Sweden.

Wawili hao wanasemekana kuwa walionana mara ya kwanza katika mkahawa mmoja mwaka wa 2010.

Image caption Maelfu ya watu walijitokeza mjini Stockholm kushudia maharusi

Japo kura za maoni zinasema kuwa umaarufu wa familia ya kifalme umedorora katika miaka ya karibuni,maelfu ya wenyeji walifurahia harusi yao kote mjini Stockholm.

Takriban wageni mashuhuri 200 walihudhuria chajio na maharusi hao katika kisiwa cha kifahari cha Skeppsholmen.

Image caption Jamaa na marafiki wa kifalme pia walihudhuria

Kabla ya wawili hao kukutana bi Hellqvist aliwahi kupigwa picha za nusu uchi na hata kupachikwa katika jarida maalum la wanaume mwaka wa 2004.