Mradi wa Suez wakaribia kufunguliwa

Mfereji wa Suez

Wakuu wa Misri wanasema njia ya pili iliyojengwa ili kupanua Mfereji wa Suez itafunguliwa Agosti.

Mradi huo wa kupanua Suez Canal umepewa uzito na Rais Abdul Fattah al-Sisi, ambaye aliamrisha kuwa umalizwe katika kipindi cha mwaka mmoja.

Mradi umegharimu dola bilioni nane na umekusudiwa kuchangamsha uchumi wa Misri ambao umezorota.

Njia hiyo piya itazidisha mara dufu idadi ya vyombo vya bahari vitavyoweza kutumia Mfereji wa Suez uliojengwa mwanzo miaka 145 iliyopita.

Wakuu wanasema mfereji huo uliotanuliwa utakuwa salama ingawa Misri inakabili tishio linalozidi la wapiganaji wenye msimamo mkali na wenye uhusiano na Islamic State.