Polio:Pakistan yatoa onyo kwa wazazi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Watoto wakipewa chanjo ya ugonjwa wa kupooza Polio nchini Pakistan

Maafisa wa utawala nchini Pakistan wametoa onyo kwa wazazi watakaokataa kuwapa watoto wao chanjo ya kupooza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Maafisa wa utawala katika jimbo kubwa zaidi nchini humo Baluchistan, wanasema kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuenea upya kwa ugonjwa huo hatari na hivyo kuwalazimu kuchukua tahadhari zaidi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wazazi wengi wanashuku kuwa chanjo hiyo ni sehemu ya njama ya mataifa ya Magharibi kupunguza idadi ya Waislamu

Kulingana na mpango huo mpya, kila mtoto atalazimika kuwa na cheti cha kuonesha kuwa tayari amepokea chanjo hiyo ya kupooza kabla ya kupokea huduma yeyote kutoka kwa serikali ikiwa ni pamoja na kuingia shuleni.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mazishi ya mhudumu wa afya aliyeuawa na waislamu wenye siasa kali

Familia nyingi zinapinga watoto wao kupokea chanjo kufuatia uvumi kuwa ni njama ya mataifa ya magharibi ya kuwahasi watoto wao kwa nia ya kupunguza idadi ya waislamu duniani.

Makundi ya kigaidi yamekuwa yakiwalenga maafisa wa afya wanaotoa chanjo hiyo wakisema kuwa inawafanya watoto kushindwa kupata watoto wakitimiza umri unaostahili.