Polisi walaumiwa kwa utepetevu Kenya

Image caption Polisi walaumiwa kwa utepetevu Kenya HRW

Shirika linalopigania haki za kibinadamu la Human Rights Watch linasema kuwa vitendo vya vikosi vya usalama nchini Kenya baada ya shambulizi la wanamgambo wa Al Shabaab katika mkoa wa pwani vilichangia kuongezeka kwa taharuki nchini humo.

Human Rights Watch inayasema hayo kwenye ripoti iliyotolewa wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja tangu wanamgambo wa Al shabaab wauvamie mji wa Mpeketoni ulioko katika eneo la Lamu pwani ya kenya na kuwaua zaidi ya watu 60.

Wengi waliouawa walikuwa wanaume ambao hawakuwa waislamu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Uharibifu uliotokea Mpeketoni

Human Rigts watch inasema kwa vikosi vya usalama vilishindwa kuwalinda raia wakati huo na punde baada ya shambulizi hilo.

Aidha HRW inasema kuwa maafisa hao walizembea ilipowadia wakati wao wa kutekeleza wajibu wao wa kufanya upelelezi wa kina ilikuzuia mashambulizi zaidi.

Hilo halikufanyika.

Haki miliki ya picha KDF
Image caption Vikosi vya Usalama nchini Kenya viliwaua wanamgambo 11 hapo jana Lamu

Vikosi vya usalama aidha vilizembea kutoa habari na hata walipoulizwa mbinu walizotumia walianza kuwadhalilisha jamii ya Waislamu na Wasomali jambo lililochangia kuongezeka kwa taharuki.

Ripoti hiyo imetolewa siku moja tu baada ya wanamgambo wa Al Shabaab kuivamia kambi ndogo ya kijeshi katika eno hilo la Lamu.