Mwanajeshi wa Korea Kaskazini atorokea Kusini

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mwanajeshi mmoja wa Korea Kaskazini atorokea Kusini

Jeshi nchini Korea Kusini linasema kuwa mwanajeshi wa Korea Kaskazini ametoroka nchi hiyo na kuingia nchini Korea Kusini akipitia mpaka wa mkoa wa Gangwo

Mwanajeshi huyo mwenye umri wa makamo alivuka mpaka huo kwa miguu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mpaka wenye ulinzi mkali wa mkoa wa Gangwo

Kuhama kwa wanajeshi kupitia mpaka huo ulio chini ya ulinzi mkali si jambo la kawaida.

Korea Kusini ilichukua hatua za kuboresha ulinzi kwenye mpaka kufuatia tukio la mwaka 2012 wakati mwanajeshi mwingine kutoka Korea Kaskazini alivuka mpaka usiku wa manane na kuingia nchini Korea Kusini.