Rais wa Sudan ameondoka Afrika Kusini

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Omar al Bashir wa Sudan

Rais Omar al Bashir wa Sudan ameondoka nchini Afrika Kusini.

Rais Bashir ameondoka akiandamana na waziri wa maswala ya kigeni wa Sudan huku ikiahidiwa kuwa watazungumza na waandishi wa habari pindi watakapotua mjini Khartoum.

Mwandishi wa BBC aliyeko Afrika Kusini Nomsa Maseko, anasema kuwa ndege ya rais al Bashir ilijazwa mafuta jana usiku na kuwekwa mstari wa mbele tayari kabisa kuondoka katika uwanja wa ndege wa kijeshi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Bashir amekuwa nchini Afrika kusini kuhudhuria kikao cha viongozi wa Umoja wa Afrika mjini Johannesburg.

Rais Bashir ameondoka licha ya kuwepo amri ya mahakama ya kumzuia kuondoka nchini humo hadi kesi dhidi yake itakaposikizwa.

Mahakama hiyo ilikuwa inapaswa kuamua ikiwa Bwana al-Bashir atakabidhiwa kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC yenye makao yake mjini Hague Uholanzi ilikukabiliana na mashtaka ya uhalifu wa kivita na mauaji yahalaiki yanayomkabili .

Majaji watatu walikuwa wanasikiza kesi hiyo rais Bashir alipopuzilia mbali amri hiyo na kuondoka.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Rais Bashir anasakwa na mahakama ya ICC kujibu tuhuma za mauaji ya halaiki katika jimbo la Darfur

Rais huyo wa Sudan amekuwa nchini Afrika kusini kuhudhuria kikao cha viongozi wa Umoja wa Afrika mjini Johannesburg.

Waziri wa mambo ya nje wa Sudan, Ibrahim al-Ghandour, amesema Bwana al-Bashir atarejea Sudan baada ya mkutano huo.

"Tupo hapa kama wageni waalikwa na serikali ya Afrika Kusini.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais Bashir alikuwa huko kwa mualiko wa rais Zuma

ma''Naamini serikali ya Afrika Kusini itaweza kukabiliana na mahakama zake na yeyote anayejaribu kumzuia Rais Bashir kuondoka nchini humu.''

''Naweza kuwaambia waziwazi kuwa Rais Bashir ataondoka kwa wakati kama ilivyokuwa imepangwa." anasema waziri huyo wa mambo ya nje wa Sudan.