Mkutano kuhusu wahamiaji wafanyika Ulaya

Haki miliki ya picha Press Association
Image caption Mkutano kuhusu wahamiaji wafanyika Ulaya

Mawaziri kutoka nchi za ulaya wanakutana nchini Luxembourg hii leo kuzungumzia mipango ya kukabiliana na maelfu ya wahamiaji wanaojaribu kuvuka bahari ya Mediterranaean kwa kutumia mashua.

Kati ya masuala wanajaribu kuzungumzia ni pamoja na mpango wa tume ya ulaya wa kugawana wahamiaji 40,000 ambao watafanikiwa kuwasili nchini Italia na Ugiriki kwa mashua kwa muda wa miaka miwili inayokuja.

Mpango huo umepingwa na nchi zingine za ulaya zinazodai kuwa wahamiaji hawatalazimishwa kwenda nchi ambazo hawana mipango ya kuishi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mkutano kuhusu wahamiaji wafanyika Ulaya

Italia na ugiriki ambazo zimeshuhudia kuwasili kwa zaidi ya watu 100,000 wanaowasili katika pwani zao mwaka huu, zinasisitiza kuwa nchini zingine za ulaya ni lazima nazo zichukue mzigo huo.

Serikali ya Italia inataka kigawanwa kwa njia iliyo sawa wahamiaji wanaowasili barani ulaya. Imesema kuwa ikiwa nchi za ulaya haziwezi kutoa usaidizi basi Italia itachukua hatua zingine ambazo ilisema hazitakuwa nzuri.