Wakurd waukomboa mji wa Tel Abyad, Syria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakimbizi wa Syria katika mji wa Tel Abyad ulio mpakani mwa Syria na Uturuki

Wapiganaji wa KiKurd, YPG, kaskazini mwa Syria wanasema wanaudhibiti kikamilifu mji wa kimkakati wa mpakani wa Tel Abyad kutoka kwa wapiganaji wa kundi la Islamic State.

Kamanda wa wanamgambo wa Kikurd, Dr Huseyin Kocher ameiambia BBC kuwa mji wa Tel Abyad unadhibitiwa kikamilifu na wapiganaji wa Kikurd.

Tuliutwaa mji huo baada ya mapigano makali, kwa kushambulia kutokea pande zote. Wapiganaji wa YPG karibu wamemaliza operesheni ya kijeshi ndani ya mji huo.

ISIS wameuawa wengi na wengi wao walikimbia kabla ya kuutwaa mji huo.Inawezekana wakawepo wapiganaji wa IS katika maeneo ya karibu lakini mapigano yamesimama kwa sasa.

Tunajua kuwa wapiganaji wa ISIS wamepanda mabomu mengi ardhini, raia waliobaki katika mji huu wako majumbani mwao na salama kwa sasa.

Huu ni mji wao na wanatakiwa watulivu. Mji wote unadhibitiwa na hakuna mapigano zaidi.

Watu wetu wafahamu kwamba tutasafisha mabaki yote ya wapiganaji wa ISIS katika mji wa Rova, kaskazini mwa Syria.