Jeb Bush kugombea urais Marekani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jeb Bush gavana wa Florida aliyetangaza kugombea urais wa Marekani 2016

Mwanasiasa wa chama cha Republican, na gavana wa jimbo la Florida, Jeb Bush ametangaza rasmi ametangaza rasmi nia yake ya kuwania nafasi ya urais wa taifa hilo kubwa duniani kiuchumi kwa tiketi ya chama hicho cha Republican.

Akizungumza katika mkutano wake wa hadhara huko Miami,Jeb ambaye baba yake na kaka yake wamewahi kuongoza Marekani ameubeza utawala wa Rais Obama katika sera zake za mambo ya nje.

Lakini mwandishi wa BBC Amerika Kaskazini anasema Jeb Bush pia anaweza kutegemea mtandao wa kisiasa wa kifamilia na nguvu ya uchangishaji.