Raia Nigeria wapinga posho za wabunge

Image caption Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria

Wananchi wa Nigeria wamechukizwa na taarifa kwamba wabunge wamejiidhinishia mamilioni ya dola kwa ajili ya posho ikiwemo ya mavazi.

Gazeti moja nchini Nigeria limesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya posho inayohusisha pia kipengele cha mavazi, kila mjumbe wa baraza la Seneti na Baraza la Wawakilishi atapokea wastani wa dola za Kimarekani laki moja katika mhula mmoja wa kipindi cha miaka minne.

Umaskini umetapakaa nchini Nigeria kwa idadi ya watu milioni mia moja wa Nigeria wakishi maisha ya chini ya dola moja kwa siku. Ujumbe mwingi umetumwa katika mitandao ya kijamii ukipinga malipo hayo.