Urusi kuimarisha zana zake za nyuklia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Urusi kuimarisha zana zake za nyuklia

Rais wa Urusi, Vladmir Putni, ametangaza kuwa Urusi itaongeza zaidi ya makombora 40 ya kinukilia yanayoweza kufikia mabara mbalimbali duniani kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Alisema kuwa makombora hayo mapya yatakuwa ya kisasa yatakayoweza kukwepa vifaa maalumu vya kukabiliana na aina zozote za silaha.

Hatua hii inaonyesha wazi kuwa Urusi imechukulia vibaya sana mazoezi ya kijeshi ambayo yameimarishwa na mataifa wanachama wa muungano wa kujihami wa NATO katika mataifa ya Poland na Baltic.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Urusi tayari imeanza kubadili silaha zake zote ili zifikie viwango vya kisasa.

Urusi inaonekana kukasirika kuwa Marekani imeanza kubadilisha maeneo yaliyoegezwa vifaru vyake na magari mengine ya kivita katika maeneo yaliyo karibu na Urusi.

Hatua ya kuanzisha mazoezi ya kijeshi katika maeneo hayo yalichukuliwa na Marekani, kufuatia hatua ya Urusi ya kujinyakulia eneo la Crimea na kuiingiza majeshi yake katika maeneo mengine ya Ukraine.

Haki miliki ya picha RIA Novossti
Image caption Hatua hii inaonyesha kuwa Urusi imechukulia vibaya mazoezi ya NATO

Katika juhudi za kuonyesha ubabe wake dhidi ya mataifa ya Magharibi kufuatia kuimarika kwa uhasama kati yao, Rais Putin ameamua kuimarisha zana zake za kinukilia.

Hatua hii inaonyesha dhahiri kuwa zana za kisasa za kivita zimeanza kupungua nchini Urusi.

Urusi tayari imeanza kubadili silaha zake zote ili zifikie viwango vya kisasa.