Wapinzani wapinga muhula wa 3 wa Kagame

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Paul Kagame wa Rwanda

Wapinzani wa rais wa Rwanda Paul Kagame wameshtumu mapendekezo ya kuifanyia mabadiliko katiba ili kumruhusu kuwania muhula wa tatu.

Zaidi ya raia milioni 7.3 wametia sahihi ombi la kuunga mkono mabadiliko hayo.

Wakosoaji wanasema wengi waliounga mkono ombi hilo ni wafungwa ambao hawaruhusiwi hata kupiga kura.

Bwana Kagame ameliongoza taifa hilo tangu mwisho wa mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Taifa jirani la Burundi limekumbwa na mgogoro tangu mwezi Aprili wakati rais Pierre Nkurunziza alipotangaza hamu yake ya kuwania muhula mwengine wa tatu.