Unyanyasaji wa Kingono marufuku:UN

Haki miliki ya picha
Image caption Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf

Ripoti ya umoja wa mataifa inasema askari waliopo katika maeneo ya kulinda amani watakaojihusisha na vitendo vya unyanyasaji wa kingono watachukuliwa hatua kali ikiwemo hatua ya kutopeleka majeshi.

Hata hivyo ripoti hiyo ambayo umoja wa mataifa uliagiza ifanyike kabla ya tukio la hivi karibuni la ukiukwaji wa kimapenzi huko Haiti na Liberia,tukio ambalo liliisababisha Liberia kutupiwa macho na dunia.

Makubaliano kwa mjibu wa ripoti hiyo ni kwamba Liberia imetazamwa kama nchi ambayo imekiuka haki za watoto na kwamba haitakiwi kupeleka majeshi yake katika vikosi vya kulinda Amani.

Wanajeshi wote ambao watabainika kwenda kinyume na kusababisha unyanyasaji wa kingono,basi hatua za kisheria dhidi yao zitachukuliwa.

Umoja wa mataifa umehimiza uchunguzi zaidi kufanyika kutokana na tuhuma hizo.