Serikali ya muungano Palestina kuvunjika

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais Mahmoud Abbas wa Palestina

Rais wa Palestina amesema kuwa serikali ya muungano kati yake na wanamgambo wa Hamas itavunjika.

Bwana Mahmud Abbas ameliambia vuguvugu lake la Fatah, kuwa lazima uhusiano huo uvunjike kwa kuwa Hamas haitairuhusu serikali yake kuendesha shughuli katika eneo la Gaza, ambako wameshikilia wao.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kiongozi wa Hamas kushoto Khaled Meshaal na rais wa Palestina Mahmoud Abbas

Serikali hiyo iliundwa mwaka uliopita na ilitarajiwa kumaliza uhasama kati ya makundi hayo mawili lakini malengo yake yamekumbwa na matatizo mengi.

Hamas wanaongoza Gaza ilhali kundi la bwana Abbas la Fatah limeshikilia maeneo ya wa Palestina ya West Bank.