Shambulio lawaua watu 9 kanisani US

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption south carolina

Polisi katika jimbo la South Carolina nchini Marekani wamesema kuwa mtu mmoja aliyejihami kwa bunduki amewapiga risasi na kuwaua watu tisa ndani ya kanisa la kimethodist.

Polisi wa eneo hilo la Charleston wameelezea kuwa kwa sasa wanamtafuta mshukiwa huyo anayeaminiwa kuwa kijana wa kizungu katika miaka ya ishirini.

Shambulio hilo limefanyika ndani ya kanisa la Emmanuel African Methodist Church, kanisa linaloaminiwa kuwa la zamani zaidi la kiafrika nchini Marekani

Polisi wamesema kuwa shambulio hili ni la chuki ya rangi ya ngozi.