Hong Kong yapinga mapendekezo ya Uchina

Haki miliki ya picha AP
Image caption Matokeo ya kura ya Hong Kong

Ingawa kutupiliwa mbali kwa mapendekezo ya serikali kuu ya Uchina kulitarajiwa huko Hong Kong utaratibu uliofuatwa uliwashangaza wengi.

Huku ikiwa zimesalia saa chache tu kabla ya kura muhimu kupigwa kuamua hatma ya siku za usoni za Hong Kong, wabunge wanaounga mkono serikali kuu ya Uchina waliomba majadiliano yasitishwe.

Waliponyimwa ombi lao waliondoka wote bungeni kwa ujumla.

Wakati maafisa wa serikali ya Hong Kong walipotoa hotuba zao ilikuwa masaa kadhaa kabla ya wakati uliowekwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kura Hong Kong

Waandishi wa habari walionekana wakisukumana wakijaribu kupata mahali pa kuketi katika eneo la bunge.

Kengele ilipigwa kuwakumbusha wabunge kuwa wakati wa kupiga kura ulikuwa umewadia.

Kulikuwa na hali ya kimya kikubwa katika bunge.

Kuna sauti iliyosikika ikiomba shughuli zote za bunge zisimamishwe huku ikiwa zimesalia dakika chache tu.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Baraza la Legco

Msimamizi wa shughuli hizo alikataa na hapo ndiposa wabunge wanaounga mkono serikali kuu walipoondoka wakilalamika.

Kwa hivyo mpango wa Serikali uliangushwa kwa kura nyingi sana bungeni.