Boko Haram lawaua watu 38 nchini Niger

Haki miliki ya picha
Image caption Niger

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram kutoka Nigeria wamewaua watu 38 katika shambulio katika vijiji viwili kusini mwa Niger.

Mbunge wa eneo hilo, Bullu Mammadu, ameiambia BBC kuwa wanawake na watoto walikuwa miongoni mwa wale waliopigwa risasi na kuuawa.

Alisema wapiganaji hao walivishambulia vijiji vya Ungumawo na Lamina Jumatano usiku na kuchoma nyumba nyingi.

Niger ni miongoni mwa mataifa yaliobuni kikosi cha kimataifa cha kukabiliana na wapiganaji hao katika eneo la magharibi mwa Afrika.