Rais Obama akerwa na mauaji Marekani

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Barack Obama wa Marekani

Rais Barak Obama amesema mauaji ya watu tisa ndani ya Kanisa la Waafrika Wamarekani katika eneo la Charleston katika jimbo la Carolina Kusini yanaibua maswali kuhusu sehemu mbaya ya historia ya Marekani.

Katika hotuba yake iliyoonyeshwa katika televisheni muda mfupi baada ya polisi kumkamata mtuhumiwa ambaye ni kijana wa kizungu-- Bwana Obama amesema chuki miongoni mwa jamii kwa misingi ya rangi na imani ni kitisho kwa demokrasia ya Marekani na misingi yake.

Amesema mauaji ya watu wengi hayatokei kwa kiasi hiki katika nchi nyingine zilizoendelea, na ametaka kufanyika kwa mabadiliko ya pamoja katika fikra za Wamarekani kuhusu ghasia zinazosababishwa na matumizi ya silaha.