Watu 30 wauawa kwa mabomu ,Yemen

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mahsmbulizi ya mabomu huko Sanaa

Mfululizo wa milipuko ya mabomu imeendelea kurushwa katika misikiti ya Shia na Ofisi zilizopo katika la jimbo la Yemen, Sanaa, na kusababisha vifo vya watu 30.

Mashambulizi hayo ya mabomu yamewalenga waumini wa Shia waliokuwa katika ibada yao ya jioni, na Ofisi ambayo yanatumiwa na kikundi cha waasi wa Houthi.

Wanamgambo wa Islamic State wamekiri kuhusika na milipuko hiyo na kudai kuwa ni hatua yao ya kulipa kisasi dhidi ya Houthi, walioteka jimbo la Yemen na milki zake.

Kwa sasa mazungumzo yanaendelea huko Geneva kati ya waasi na Serikali,huku maofisa wa umoja wa mataifa wakijaribu kusuluhisha pande hizo mbili ili kusitisha mapigano