Wabunge waomba msamaha Hong Kong

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wabunge wa Hong Kong

Kundi la Wabunge wa Hong Kong wamenunua nafasi katika magazeti ya eneo hilo na kuwaomba wapiga kura msamaha kwa kukosa kuwepo wakati kura muhimu ya kuamua hatma ya kidemokrasia ya eneo hilo ilipopigwa bungeni siku ya alhamisi.

Wabunge hao ni wale waliokuwa wanaunga mkono Serikali Kuu ya Uchina kuamua ni nani anayepaswa kugombea kiti wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Wabunge hao waliondoka bungeni kabla ya kura hiyo kupigwa katika juhudi za kuchelewesha uamuzi wa kupinga Uchina.

Hata hivyo hatua yao haikusaidia lolote kwa sababu wabunge wanaopinga Serikali kuu walishinda kwa wingi wa kura kuliko ilivyotarajiwa.