Pikipiki ya kielektroniki kuuzwa Taiwan

Haki miliki ya picha
Image caption smart scooter

Pikipiki ya kielektroniki ilio na betri zinazoweza kubadilishwa inatarajiwa kuuzwa nchini Taiwan kwa bei ya dola 4,140.

Pikipiki hizo zilizotengezwa na Gogoro zitapatikana kwa uagizaji mjini Taipei kuanzia tarehe 27 mwezi Juni ,kampuni hiyo imetangaza.

Waendeshaji wake watakuwa na fursa ya kubadilisha betri katika vituo kadhaa vya kuchaji betri hizo vya Gogoro mjini humo.

Hiyo ndio njia ya kipekee watakayoweza kuzichaji pikipiki hizo ,na kuwawacha wamiliki wake wakisalia kuwa katika mtandao wa watengezaji wake pamoja na mipango yake ya bei.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption smartscooter

Na kufuatia hatua hiyo wamiliki wa pikipiki hizo watapewa mwaka mmoja wa bima ya wizi,miaka miwili ya uangalizi wa pikipiki pamoja na miaka miwili ya kuchaji bure betri hizo katika vituo hivyo.

Pikipiki hizo zinaendeshwa kwa kutegemea betri mbili zinazoweza kutolewa na ambazo huzipatia uwezo wa kuendeshwa kwa kilomita 97 bila betri kuisha.

Gogoro imesema kuwa watumizi wake wataweza kubadilisha betri kwa sekunde tu.