Misa ya waliouawa yafanyika Charleston

Haki miliki ya picha
Image caption Misa ya waliouawa yafanyika Charleston

Maelfu ya watu wamehudhuria misa katika mji wa Charleston jimbo la South Carolina nchini Marekani kuwakumbuka waamerika tisa weusi ambao waliuawa kwa kupigwa risasii na jamaa mmoja mzungu walipokuwa kwenye mafunzo kanisani.

Wakishikana mikono waombolezaji waliimba nyimbo za kujifariji. Viongozi wa wakirsto na wayahudia wametaka kuwepo amani.

Haki miliki ya picha
Image caption Mshukiwa Dylann Roof

Mapema mshukiwa Dylann Roof alifikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka tisa ya mauaji

Mmoja wa marafiki zake Christon Scriven aliiambia bbc kuwa, Roof alikuwa amesema kuwa angewaua wanafunzi katika chuo kilicho karibu lakini alitulia baada ya kuhojiwa .