Watu 74 wafariki kwa kunywa pombe India

Image caption Waathiriwa wa pombe ya sumu India

Wakaazi wa eneo la maskini la mjini Mumbai, India, wanaomboleza baada ya watu kadhaa kufa kutokana na pombe iliyokuwa na sumu.

Polisi wanasema watu waliokufa kutokana na pombe ya kienyeji iliyokuwa na sumu idadi imeongezeka na kufikia 74.

Image caption watu 74 wamefariki kutokana na pombe hiyo

Wengine ni mahtuti.

Watu kadha wamekamatwa kwa kuuza pombe hiyo, na polisi wanane wamesimamishwa kazi kwa muda, wakituhumiwa kuwa waliruhusu pombe hiyo kuuzwa katika eneo lao.