Wauawa katika duka la pombe Mexico

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uvamizi wa duka la pombe nchini Mexico

Watu waliokuwa na silaha wamevamia duka moja la pombe nchini Mexico ambapo watu 10 waliuawa.

Wavamizi hao waliwasili kwa magari mawili na kuwafyatulia risasi wateja waliokuwa ndani ya duka hilo katika mji ulio kaskazini wa Garcia.

Kisha miili yao ilivuliwa nguo na kuporwa.

Wachunguzi wanadai kuwa wanaume hao walikuwa wamelengwa makusudi na mauaji hayo huenda yanahusiana na tofauti kati ya makundi hasimu.