Waingereza wapinga mbano wa matumizi

Maandamano mjini London Haki miliki ya picha Getty

Maelfu ya watu wa Uingereza waandamana mjini London kupinga mpango wa serikali wa kubana matumizi.

Maandamano hayo yanajumuisha wafuasi wa vyama vya wafanyakazi, wanasiasa, wanaopinga vita pamoja na watu maarufu.

Waratibu wanasema watu wamekerwa kuwa wao wanapita kwenye shida kwa sababu ya msukosuko ambao wao siyo sababu.

Wanasema kuwa maandaano hayo - kutoka mitaa ya soko la fedha hadi bungeni - ni mwanzo wa kampeni ya maandamano nchi nzima.