Vibonzo vya mtume Uholanzi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Geert Wilders

Mwanasiasa wa mrengo wa kulia nchini Uholanzi Geert Wilders anasema kuwa atapeperusha picha za vibonzo vya kumhusu mtume Mohammed katika kituo cha runinga cha taifa nchini Uholanzi hii leo.

Anatumia muda uliotengewa vyama vya kisiasa.

Vibonzo hivyo ni vile vilivyoonyeshwa katika warsha moja wa jimbo la Texas nchini Marekani mwezi uliopita wakati watu wawili waliuawa na walinda usalama.

Bwana Wilders alikuuwa mzungumzaji kati tamasha hilo.

Matangazo ya vibonzo hivyo yanafanyika wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na balozi zote za Uholanzi kote dunia zimewekwa katika hali ya tahadhari.