Mwandishi wa aljazeera akamatwa Ujerumani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aljazeera

Kituo cha runinga cha Al Jazeera kinasema kuwa mmoja wa waandishi wake wa habari amekamatwa nchini Ujerumani kufuatia ombi la Misri.

Ahmed Mansour, ambaye anafanya kazi na idhaa ya kiarabu ya al Jazeera alizuliwa alipojaribu kupanda ndege kutoka Berlin kwenda nchini Qatar.

Polisi nchini Ujerumani wanasema kuwa bwana Mansour amezuiliwa kufuatia waranti ya kimataifa ya kutaka akamatwe kutoka kwa utawala nchini Misri.

Mahakama nchini Misri ilimhukumu Mansour kifungo cha miaka 15 jela kutokana na mashtaka ya mateso.

Aljazeera imeyataja mashtaka hayo kuwa ya uongo.