Ibada ya maombolezo Charleston

Haki miliki ya picha epa
Image caption Waumini wakiwa katika ibada huko Charleston

Mamia ya Waumini wamehudhuria ibada ya mazishi ya watu tisa waliouawa katika kanisa moja lililopo katika mji Charleston nchini Marekani wiki iliyopita.

Watu wengi kutoka maeneo ya jirani walikusanyika nje ya kanisa hilo kushiriki misa hiyo ya maombolezo. Ilikuwa ni ibada ya kwanza kanisani hapo tangu siku ya Jumatano iliyopita kulipofanyika shambulio hilo.

Mmoja ya waliouawa alikuwa ni mchungaji Clementa Pinckney. Viongozi wa kanisa wamesema shetani aliingia kanisani hapo siku hiyo ya Jumatano, lakini alishindwa. Waumini nao wametoa maoni yao:Nimeshukuru kuona ibada ni ya kutia moyo, imetia moyo sana na neno alilotoa mchungaji ni mahala pake haswa. Ni kile ambacho watu wanakihitaji leo, linalotufanya tujue kwamba hata iwe vipi mungu bado yuko katika ufalme wake....''

Imenifanya nihisi kwamba kuna mambo mengi yanaendelea siku hizi katika fikra za watu na kuhisi kwamba kuna ushirikiano na matumaini kwamba tutaungana pamoja kushinda vile ilivyokuwa awali.......