Watu waliofariki na pombe India wafika 90

Haki miliki ya picha AFP
Image caption India

Zaidi ya watu 90 wamefariki kutokana na pombe iliokuwa na sumu katika mji wa India, Mumbai huku wengi wengine wakiwa hospitalini.

Vifo vya kwanza viliripotiwa siku ya jumatano.

Naibu wa kamishna wa polisi katika mji huo amesema kuwa watu 150 waliokunywa pombe hiyo iliotengezwa nyumbani katika mtaa mmoja wa mabanda.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption India pombe

Vifo vinavyosababishwa na pombe ilio na sumu vimekuwa jambo la kawaida nchini India ambapo pombe rahisi inayotengezwa nyumbani ni maarufu miongoni mwa wakaazi wake walio maskini.