Kijana amjeruhi polisi wa Israel

Image caption Polisi

Askari polisi mmoja wa Israel, ameumia vibaya aliposhambuliwa kwa kisu katika eneo la mashariki mwa Jerusalem, ambalo linakaliwa na Israel.

Polisi wa Israel wanasema, walimpiga risasi na kumjeruhi kijana mdogo wa Kipalestina, aliyefanya shambulio.

Jambo hilo limetokea nje ya lango la asili, la Damascus Gate, la kuingilia mji wa kale.

Siku mbili zilizopita, mwanamume aliyekuwa na silaha, alimpiga risasi na kumuua mwanamume wa Israel, na kumjeruhi mwengine, katika ufukwe wa magharibi, unaokaliwa.