Visa 3 vya MERS vyaripotiwa K Kusini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mgonjwa wa Mers

Maafisa wa afya nchini Korea kusini wamethibitisha visa vingine vitatu vya ugonjwa wa matatizo ya kupumua au MERS.

Kati ya wale waliopatikana wakiwa na ugonjwa huo ni pamoja na daktari katika hospitali moja mjini Seoul ambaye ametajwa kuwa kitovu cha ugonjwa huo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mers korea kusini

Wataalam wanasema kuwa visa vyote 170 vilitoka kwenye mahospitali na hakuna maambukizi yoyote katika maeneo wanakoishi watu.

Watu 25 wameaga dunia tangu mlipuko wa ugonjwa huo kuripotiwa barani Asia mwezi uliopita.