Shambulizi la bunge Afghanistan lasitishwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bunge

Serikali ya Afghanistan inasema kuwa imefanikiwa kusitisha shambulio katika bunge na kuweza kuwaua washambuliaji wote.

Kundi la wapiganaji wa Taleban limekiri kutekeleza shambulio hilo ambalo lilianza na kulipuka kwa gari lililotegwa vilipuzi nje ya bunge kabla ya ufyatuzi wa roketi na risasi.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bunge

Hatahivyo wapiganaji hao walishindwa kuingia ndani ya jengo la bunge.

Msemaji wa wizara ya ndani amesema kuwa hakuna mbunge aliyejeruhiwa lakini zaidi ya watu 20 walijeruhiwa na vigae vya chupa.

Afisa mmoja wa wizara ya afya amesema kuwa mmoja ya waliojeruhiwa alikuwa katika hali mbaya.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shambulizi Afghanistan

Shambulizi hilo lilifanyika wakati bunge lilipokutana ili kumchagua waziri mpya wa ulinzi.