Sherehe ya nyama ya mbwa Uchina yapingwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uchina

Sherehe ya kula nyama ya mbwa kusini magharibi mwa China imeanza huku kukiwa na pingamizi miongoni mwa wanaharakati wa haki za wanyama.

Takriban mbwa 10,000 watachinjwa na nyama yao kuliwa katika sherehe hizo zitakazofanyika katika eneo la Yulin mkoa wa Guangxi siku ya jumapili na jumatatu ili kuadhimisha kuanza kwa msimu wa joto kulingana na vyombo vya habari vya kitaifa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uchina

Mwalimu mmoja aliyestaafu kutoka Tianjin aligonga vyombo vya habari alipowanunua mbwa wengi ili kuwanusuru

Wakaazi na wafanyibiashara huko Yulin wanasema kuwa wanyama hao huuawa kwa njia nzuri.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uchina

Wanaharakati wanasema kuwa mauaji hayo ni ya kikatili na kwamba kampeni ya mitandaoni ya kupiga marufuku sherehe hiyo imetiwa sahihi na zaidi ya watu milioni 3.8 kufikia sasa na kampeni hiyo kuungwa mkono na watu wengi mwaka huu kutoka watu maarufu wa kitaifa na kimataifa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nyama ya mbwa

Watu maarufu akiwemo mcheshi wa Uingereza Ricky Gervais wamezungumza katika mtandao wa Twitter na alama ya reli StopYuLin2015.

Nyota wa muziki nchini Uchina Chen Kun na msanii Yang Mi wamesema kuwa wanaiunga mkono kampeni hiyo katika mtandao wa Weibo.