Nuklia:Iran yatakiwa kuweka juhudi zaidi.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Iran nuklia

Uingereza imesema kuwa Iran inahitaji kujizatiti zaidi iwapo inataka kuafikia mkataba kuhusu mpango wake wa kinuklia.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Uingereza Phillip Hammond amesema kuwa angependelea kuona hatua zinapigwa hivi karibuni na kuongezea kuwa mda wa mazungumzo hayo unaweza kuongezwa baada ya kukamilika kwa mda uliowekwa mwishoni mwa mwezi huu.

Amesema kuwa atakutana na mkuu wa sera za bara Ulaya pamoja na wenzake kutoka Ujerumani,Ufaransa na Iran.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Iran

Siku ya jumapili bunge la Iran liliondoa uwezo wake wa kuzuia makubaliano na mataifa sita yenye uwezo mkubwa duniani.

Iran ilikubaliana na wazungumzaji wa kimataifa kutoka Marekani,China,Ujerumani,Uingereza Ufaransa na Urusi mnamo mwezi Aprili.