Apple music yabadili sera yake ya malipo

Haki miliki ya picha AP
Image caption Apple

Huduma ya Apple music imebadilisha sera ya malipo yake ,siku moja baada ya msanii Taylor Swift kusema kuwa ataizuia kampuni hiyo kucheza mziki wa albamu yake 1989.

Katika barua ya wazi kwa kampuni ya Apple,Swift amesema kwamba anaizuia albamu hiyo kwa kuwa hapendelei vile walipaji wa muziki hupewa uhuru wa kusikiliza nyimbo bure kwa miezi mitatu kama jaribio.

Lakini sasa Apple imesema kuwa itawalipa waasanii kwa muziki utakaochezwa mtandaoni wakati wa majaribio.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Taylor Swift

Swift alisema kuwa mpango huo si wa haki kwa kuwa Apple ina fedha ya kulipia gharama zote.

''Miezi mitatu ni mingi sana kwa msanii kukaa bila kulipwa.hatujataka kupewa simu za bure za iphone kwa hivyo tafadhali musichukue muziki wetu bila malipo'',alisema Swift.