Malaria yaua watu Guinea

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wafanyakazi wa sekta ya afya wakiuondoa mwili wa mtu aliyekufa kwa ebola.

Watafiti wa magonjwa wanasema kwamba janga kubwa la ugonjwa wa ebola nchini Guinea linazidi kuongeza idadi ya vifo vya watu wanaofariki dunia kwa maradhi ya malaria .

Utafiti huo,uliochapishwa katika jarida moja la magonjwa ya kuambukiza nchini humo,linakadiria kwamba watu wapatao elfu sabini na watano wanaougua ugonjwa wa malaria hawakupatiwa dawa, pengine kutokana na kufungwa kwa vituo vya afya,ama pengine wagonjwa walikuwa wana hofu kubwa ya kutafuta msaada wa kitabibu.

Watafiti hao wanasema magonjwa yote mawili,malaria na ebola husababisha ho

ma na hofu pia inaweza kuchangia mgonjwa kutomwona daktari.

Watafiti hao wameendelea kueleza kwamba,idadi ya wagonjwa wa malaria nchini Guinea imeshuka katika baadhi ya maeneo kwa asilia sabini .

.