Mwaka 1 tangu miraa ipigwe Marufuku Ulaya

Image caption Mwaka 1 tangu miraa ipigwe Maruku Ulaya

Ni mwaka mmoja tangu serikali ya Uingereza kupiga marufuku uuzaji na utumiaji wa miraa ama Mirungi nchini humo.

Hatua ambayo ilipokelewa kwa hisia tofauti miongoni mwa wadau wa zao hilo nchini Kenya.

Haki miliki ya picha Other
Image caption Wauzaji wa Miraa wa kimataifa

Wakulima wa zao la miraa au 'mairungi' Mashariki mwa Kenya, wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha, baada ya mmea huo kupigwa marufuku nchini Uingereza.

Mji wa Maua ambao zamani ulikuwa wenye shughuli nyingi na ulio kilomita 450 Mashariki mwa jiji kuu la Kenya, Nairobi, ni sasa umesalia na upweke.

Maduka kadhaa yamefungwa, mamia ya vijana wakikaa bila ya kufanya lolote kandokando mwa barabara wakitafuta ''mairungi'' huku wakishindwa la kufanya huku wasijue kilichowapata.

Image caption Wakulima wa zao hilo walalamika

Katika barabara muhimu wa mji huo vijana wachache mno wanaonekana wakichambua chambua zao hilo tayari kuzisafirisha hadi katika miji kadhaa ya Kenya na katika taifa jirani la Somalia.

Fatma Hussein, mama wa watoto sita amekuwa akiishi katika mji wa mauwa uliozungukwa na milima kwa miaka kumi na tano iliyopita wakinunua miraa kutoka kwa wakulima na kisha kusafirisha hadi Uingereza na Somalia.

Lakini tangu mwaka jana pale marufuku ilipotolewa kwa zao hilo, anasema kuwa biashara yake imesambaratika kabisa.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wauzaji Miraa wamepata hasara kubwa wengi wameshindwa kulipa madeni yao

''Siwezi hata kuwalipia watoto wangu karo, fedha kidogo ninayopata haiwezi kabisa kumudu kuwanunulia watoto wangu chakula''

Mita chache kutoka hapo mkenya mwingine mwenye asili ya Somali, anaendelea kusimamia kundi la vijana watano wanaopakia mzigo wa mairungi kwenye gari ili isafirishwe hadi Nairobi.

Sawa tu na mama Fatma, Mohammed Hussein anasema kuwa marufuku hiyo imewaathiri pakubwa.

'' Miaka mitatu iliyopita nilichukua mkopo kutoka katika benki moja Nchini ili kupanua biashara yangu na nikanunua magari kadhaa ya kusafirisha mairungi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kundi la Al Shabaab nalo likaongeza ushuru kwa 'mairungi' yanayoingizwa mjini Mogadishu.

Lakini mwaka mmoja baadaye, tulishtuliwa mno, hakuna tena kuuza miraa nchini Uingereza.'

Nililazimika kuyauza magari hayo kwa bei ya kutupa ili nilipe deni la mkopo'' Alisema Hussein.

Kwa sasa wafanyibiashara wengi wanategemea soko la Kenya na Somalia, lakini hivi majuzi, taifa la Somalia nalo likaongeza ushuru kwa mairungi yanayoingizwa mjini Mogadishu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wauzaji Miraa wakichagua kulingana na ubora wake

Hussein anasema kuwa kutokana na kuongezeka kwa ushuru nchini Somalia, faida kutokana na biashara yao imeshuka mno.

''Mbali na ongezeko la ushuru, pia kuna changamoto kubwa nchini humo, tangu kundi la wanamgambo wa Al Shaabab pia walipoongeza ushuru kwa wafanyibiashara wa reja reja wanaouza mairungi nchini humo, na kuwalazimisha wafanyabiashara wengi nje ya jiji kuu Mogadishu, kukimbilia maeneo mengine au hata kuachana kabisa na biashara hiyo.

Akaongeza Added Hussein.

Haki miliki ya picha
Image caption Mji wa Maua Kenya unaotegemea zao hilo kwa uchumi wake

Wapiganaji hao kadhalika walipiga marufuiku kabisa uuzaji wa mairungi katika maeneo wanayodhibiti.

Zao hilo ambalo hukuzwa tu maeneo ya Meru na viunga vyake, ni tegemeo kubwa kwa uchumi wa eneo hilo.

Takwimu kutoka kwa mamlaka inayosimamia mimea inayouzwa nje ya nchi, HCDA inaonesha kuwa zaidi ya kilo 550,948 za 'mairungi' iliuzwa nje ya nchi mwaka 2012.