Tsarnaev aomba radhi waathirika

Haki miliki ya picha AP
Image caption Picha ya utambuzi wa Tsarnayev

Dzhokhar Tsarnaev aliyefanya shambulio la bomu katika mbio za marathon mjini Boston ameomba radhi kwa waathirika wa tukio hilo.

Tsarnaev mwenye umri wa miaka 21 akizungumza mbele ya mahakama kabla ya kuhukumia adhabu ya kifo,amesema alikuwa kusikiliza kila mtu ambaye alizungumza kama shahidi wa tukio hilo, yeye mwenyewe alibainisha nguvu, uvumilivu na heshima ya waathirika. Kufuatia kauli, ya hakimu (George O'Toole) alinukuu mstari kutoka katika mashairi ya Shakespeare: '' uovu uliofanywa utaishi baada ya wao , uzuri walizika mifupa yao ''.

Watu watatu waliuawa na zaidi ya wengine mia mbili na sitini-walijeruhiwa katika shambulio hilo miaka miwili iliyopita.Dzhokhar Tsarnaev pia anahatia ya kusababisha kifo cha afisa wa polisi kwa risasi siku tatu baada ya mashambulizi ya marathon.