Burundi upinzani kususia uchaguzi mkuu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ban Ki-Moon ametoa wito kwa utawala wa nchi hiyo kuhairisha uchaguzi mkuu

Nchini Burundi hali ya kisiasa inaendelea kutokota, huku vyama vya upinzani vikitangaza kususia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuanza wiki ijayo.

Makundi ya asasi za kiraia yamewaomba raia wa nchi hio kususia kura hio, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akitaka uchaguzi mkuu wa Burundi kuahirishwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Nkurunziza amekataa kujiondoa katika uchaguzi wa urais

Makundi ya kutetea haki za kibinadamu nchini Burundi yametoa wito kwa wapiga kura nchini humo kususia uchaguzi wa ubunge unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu.

Mashirika hayo yamesema kuwa kwa sasa mazingira ya kisiasa nchini humo hayawezi kuruhusu uchaguzi huru na wa haki, kufuatia miezi kadhaa ya ghasia.

Image caption Umoja wa mataifa umekuwa ukiendesha jitihada za kuleta uwiano kabla ya uchaguzi

Makundi hayo ya kijamii yametoa taarifa ya pamoja yakitoa wito kwa jamii ya Kimataifa kutotambua uhalali wa uchaguzi huo.

Wakati huo huo katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa utawala wa nchi hiyo kuhairisha uchaguzi mkuu baada ya vyama vya upinzani kutangaza kuwa havitashiriki.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Makamu wa Rais alitoroka nchini humo baada ya kumpinga rais Nkurunziza

Takriban zaidi ya watu 50 wameuawa nchini Burundi tangu mwezi Aprili mwaka huu wakati rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kuwa atawania muhula wa tatu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waandamanaji wanapinga rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu

Maelfu ya raia wengine wa Burundi nao wamehamia mataifa jirani kwa hofu ya kuzuka mamchafuko zaidi.

Uchaguzi wa ubunge unatarajiwa siku ya Jumatatu huku uchaguzi wa urais ukipangiwa kufanyika tarehe 15 Julai mwaka huu.