Waeritrea waandamana kupinga udhalimu

Image caption Waeritrea waandamana nchini Ethiopia kupinga udhalimu chini ya Rais Afeworki

Mamia ya wakimbizi wa Eritrea wanaoishi nchini Ethiopia wameandamana mbele ya majengo ya muungano wa afrika AU wakiitaka muungano huo kuchukua hatua zaidi kumaliza ukiukaji wa haki za kibinadamu nchini mwao.

Image caption Wanaitaka muungano wa Afrika kuchukua hatua za kupunguza udhalimu nchini Eritrea

Wakiwa wamebeba mabango ya kumkashifu rais wa nchi hiyo, Isaias Afeworki, waandamanaji hao wamesema ukiukaji mkubwa wa haki zao umeendelea nchini Eritrea huku jamii ya kimataifa ikijikokota kuingilia kati.

Image caption Ripoti ya UN inasema kuwa nci hiyo inatawaliwa kwa hofu

Ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa imesema nchi hiyo inatawaliwa kwa hofu na woga mwingi.

Kiongozi wa uchunguzi wa umoja wa mataifa ameitaka mahakama ya makosa makuu ya kivita ICC kuchunguza tuhuma dhidi ya utawala wa rais Afeworki.