Mtu mmoja amechinjwa Ufaransa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mtu mmoja amechinjwa Ufaransa

Mtu mmoja amechinjwa na mwengine akajeruhiwa vibaya baada ya shambulizi la kiislamu katika mji wa Lyon Ufaransa.

Vilipuzi kadhaa vilitegwa katika karakana moja iliyoko Saint-Quentin-Fallavier

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanaume mmoja amekamatwa na maafisa wa usalama kufuatia tukio hilo.

Mvamizi aliyetekeleza mauaji hayo anasemekana kuwa alikuwa akipeperusha kibendera cha wanamgambo wa kiislamu.

Kibendera hicho kilipatikana kimetupwa karibu na eneo la tukio.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Inaaminika kuwa waliotekeleza shambulizi hao walikuwa na bendera iliyoandikwa katika kiarabu

Mwanaume mmoja amekamatwa na maafisa wa usalama kufuatia tukio hilo.

Waziri wa usalama wa ndani Bernard Cazeneuve yuko njiani kuelekea kwenye eneo la tukio.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hili ni shambulizi la kwanza tangu watu 17 wauawe miezi sita iliyopita

nza nWakati huohuo rais wa Ufaransa Francois Hollande anatarajiwa kukatiza ziara yake rasmi ya viongozi wa bara ulaya na kurejea nyumbani kukabili janga hilo.

Shambulizi hili ni la kwanza tangu lile la kigaidi lililopelekea kuuawa kwa watu 17 miezi sita iliyopita.