Viongozi wa EU wajadili wahamiaji

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wahamiaji wamekuwa wakihatarisha maisha yao kwa kusafiri kwa kutumia vyombo duni vya baharini

Viongozi wa nchi za ulaya wanakutana jijini Brussels kujadili namna ya kupambana na wimbi la wahamiaji wanaoingia nchi za Umoja wa ulaya kinyume na utaratibu.

Hakuna makubaliano yeyote yaliyofikiwa na nchi hizo katika kutatua tatizo hilo.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa mpango wa kujitolea wa kuwapokea wanaotafuta hifadhi nchini Italia na Ugiriki huenda ukapitishwa.

Mgogoro wa madeni unaokumba Ugiriki pia ni moja ya ajenda za mkutano. Awali Ugiriki na wakopeshaji wa kimataifa walishindwa kukubaliana kuhusu hatua za kuchukua kuhusu namna ya kulipa madeni yake.

Mkutano huo pia utajadili kuhusu mapendekezo ya Uingereza kuhusu Umoja wa ulaya kufanyiwa marekebisho, wakati huu ambapo uingereza inapotarajia kupiga kura ya maoni kubaki au kuondoka kwenye jumuia ya Ulaya.