Marikana:Shinikizo mkuu wa polisi afutwe kazi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Marikana:Shinikizo mkuu wa polisi afutwe

Upinzani nchini Afrika Kusini unaitaka serikali imfute kazi mkuu wa polisi Riah Phiyega baada ya tume maalum ya uchunguzi wa mauaji ya wachimba mgodi wa Marikana 2012 kumlaumu yeye na idara ya polisi kwa kusababisha vifo hivyo.

"ripoti hiyo iliwanyoshea kidole cha lawama polisi na haswa Riah Phiyega kwa kuchukua hatua ambayo walifahamu fika kuwa ingesababisha maafa"

Kiongozi wa chama cha upinzani Democratic Alliance Mmusi Maimane alisema katika taarifa hiyo.

Chama cha ''The Congress of the People'' (Cope) kilisema kuwa Phiyega hafai kuendelea kuhudumu ''ilihali maafisa wa polisi walidanganya mara mbili jopo hilo ''

Image caption Upinzani nchini Afrika Kusini unaitaka serikali imfute kazi mkuu wa polisi Riah Phiyega kufuatia mauaji ya wachimba migodi wa Marikana

Mauaji hayo yalitajwa kuwa mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo tangu ijinyakulie uhuru wake miaka 20 iliyopita.

Rais Jacob Zuma ameliita tukio hilo kuwa baya zaidi kuwahi kutekelezwa na polisi na kusema kuwa halina nafasi katika demokrasia ya taifa hilo.

Wafanyakazi wa mgodi waligoma kwa siku kadhaa,na watu 10 tayari walipoteza maisha wakiwemo watu ambao hawakuwa kwenye mgomo huo , walinzi wa mgodi na polisi, kabla ya tukio hilo la tarehe 16 Agosti.